16 Days of Activism - Remarks by Ambassador Gilsenan
Ambassador Gilsenan Launches 16 Days of Activism on Violence against Women in Mwanza Region on 25th November 2015
Speech of Ambassador Gilsenan at the launch of the 16 Days of Activism on Violence against Women in Mwanza Region.
National Theme 2015:
Hoja za kuzungumza wakati wa Uzinduzi wa Siku 16 za Harakati kuhusu Ukatili Dhidi ya Wanawake katika Mkoa wa Mwanza 25 November 2015
Kauli Mbiu ya Kitaifa 2015:
“Funguka! Chukua Hatua Mlinde Mtoto Apate Elimu”
Open Up! Take Action, Protect the child to Access Safe Education
Kama balozi wa Ireland nchini Tanzania, ninayo furaha sana kualikwa kuwa na wana Mwanza siku ya leo kuadhimisha Siku ya Kimataifa kwa ajili ya kuondoa Ukatili dhidi ya wanawake na kuzindua siku 16 za harakati dhidi ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Ninayo furaha zaidi, hasa kwa Ireland ina bahati ya kuwa na mshirika hapa jijini Mwanza, Shirika la Kutetea Haki za Wanawake-Kivulini, ambapo uzoefu wao unaonyesha kwamba kinga inaweza kufanya kazi, na kwamba inawezekana kubadili mitazamo na tabia ambazo zinaendeleza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana.
Mwaka jana, wakati wa siku 16 za Harakati juu ya ukatili dhidi ya wanawake, ilikuwa ni heshima yangu kuwa mwenyeji tukio hilo jijini Dar es Salaam ambapo Kivulini walitoa uzoefu wao katika kuhamasisha jamii ili kuzuia ukatili dhidi ya wanawake. Ujumbe muhimu kutoka kwenye tukio hili ni kwamba Ukatili Unazuilika!
Lakini inahitaji mabadiliko katika mtazamo na tabia. Hili linaweza tu kutokea pale ambapo kuna uwazi katika kufanya mjadala na mdahalo, hata kama wakati mwingine, masuala mengi ya msingi yanayohusu ukatili dhidi ya wanawake na wasichana yanaonekana kuwa ni ya kibinafsi au hata mwiko. Hii inahitaji ujasiri na uwazi mkubwa.
Ukatili dhidi ya wanawake na wasichana hutokea kila mahali, ni tatizo la dunia nzima na mmoja katika kila wanawake watatu hupitia na ukatili katika maisha yao. Inaelezewa kama "tatizo la kimataifa la afya ya umma wa la kiwango ambacho ni janga".
Kwa hapa nchini Tanzania pia ni wa kiwango cha hatari, na wa juu zaidi ya kiwango cha wastani cha kimataifa.
Kaulimbiu ya mwaka huu ni “Funguka! Chukua Hatua Mlinde Mtoto Apate Elimu”
Elimu inaweza kutumika ili kuwawezesha wasichana na wavulana na kuchangia katika kujenga mahusiano ya heshima baina yao. Shule zinaweza kuwa mahali salama ambapo watoto wanajisikia salama na wanaweza kusoma na kujifunza bila hofu ya vurugu na ukatili. Vilevile mazingira shule yanaweza kuakisi desturi za jinsia na kijamii ambazo zinaendeleza ukatili pia shule inaweza kuwa mahali pa ukatili.
Kwa bahati mbaya, kwa sasa shule za dunia nzima, na pia katika Tanzania, ni kigezo kinachochangia badala ya kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Baadhi ya maeneo ambayo ukatili wa kijinsia hutokea zaidi kwa wavulana na wasichana nchini Tanzania ni wakati wa kusafiri kwenda au kutoka shule au katika maeneo ya shule. Utafiti wa kitaifa juu ya Ukatili dhidi ya Watoto uliofanyika mwaka elfu mbili na tisa uligundua kwamba asimilia arobini na moja nukta nne ya wasichana walitaja kupitia tukio angalau moja la kuguswa bila kupenda au jaribio la ngono katika maeneo ya shule, au wakati walipokuwa njiani kwenda au kutoka shule.
Hii inatisha, kama makala ya hivi karibuni ya UNESCO ilionesha madhara makubwa ya ukatili wa kijinsia unaofanyika mashuleni ambao unachangia unawanyima watoto wa Kitanzania haki yao ya elimu.
Ndoa za utotoni
Ndoa za utotoni zinaweza kuwa na athari mbaya kwa mafanikio ya kielimu na Tanzania ni miongoni mwa nchi zinayoongoza duniani kwa idadi kubwa ya ndoa za utotoni.
Utafiti uliofanywa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) mkoani Shinyanga uligundua kwamba ni kawaida kwa wasichana kushinikizwa na kulazimishwa kufanya vibaya katika mitihani yao ya elimu ya msingi ili wasiweze kuendelea na elimu ya sekondari na kuziruhusu familia zao kuwalazimisha kuolewa. Katika baadhi ya matukio, familia hulazimisha wasichana kuacha shule ili kuolewa. Wasichana wanaolazimishwa katika ndoa za utotoni kwa kawaida wanakabiliwa na ukatili wa kijinsia na waume zao.
Kuwabakisha wasichana shuleni ni muhimu katika kuzuia ndoa za utotoni. Wasichana wenye elimu ya sekondari wana hadi zaidi ya chini ya mara sita ya uwezekano wa kuolewa wakiwa watoto, hali inayofanya elimu kuwa moja ya mikakati bora ya kuwalinda wasichana na kupambana na ndoa za utotoni.
Mimba za Utotoni
Kwa mujibu wa Utafiti wa Afya nchini Tanzania, robo ya wanawake wenye umri wa miaka 15 hadi 19 ni wajamzito au wamejifungua; na moja ya sababu kubwa ya vifo kwa wasichana hawa nchini Tanzania ni matatizo ya wakati wa kujifungua. Ni ukweli kwamba wasichana wadogo wenye chini ya 15 wana hadi mara tano zaidi ya uwezekano wa kufa wakati wa kujifungua kuliko wanawake walio kwenye miaka Zaidi ya 20.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Wizara ya Elimu nchini Tanzania, zaidi ya wasichana 16,000 wameacha shule kati ya mwaka 2008-2010 kutokana na mimba. Katika hali nyingi, wasichana wadogo hujikuta wanashindwa kumaliza masomo yao kutokana na shinikizo la familia kuolewa, unyanyasaji wa kingono, au mimba zisizotarajiwa.
Serikali na jamii ina jukumu la ziada kwa ujumla katika kuhamasisha na kusaidia wasichana, ambao wanaacha shule kwa sababu ya mimba, waweze kurudi katika mfumo wa elimu mapema iwezekanavyo mara baada ya kujifungua. Mimba haipaswi kuzuia wasichana kumaliza elimu yao. Kiuhalisia, jukumu la kumlea mtoto ni sababu ya kumwezesha Mama kubakia shuleni, ili apate elimu na aweze kuwa huru kiuchumi na kujenga maisha yake ya baadae.
Ukatili na Madhara yake katika Kujifunza
Kuna ushahidi kwamba watoto wanaoshuhudia au kupitia ukatili nyumbani wanaathirika kielimu, na viwango vya juu ya kurudia madarasa na kuacha shule.
Kwa hiyo kuna mzunguko wa matatizo ambapo wasichana ambao wameshuhudia au wamepitia ukatili wakiwa watoto wapo katika hatari zaidi kukabiliwa na unyanyasaji wakiwa watu wazima. Tunahitaji kuvunja mzunguko huu na inanipa faraja sana kuona uongozi wa Mkoa wanakabiliana na hii.
Daima huwa ninaguswa ninaposhuhudia kujitoa na uongozi kutoka kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, asasi za mashirika ya kiraia, jamii na wanawake na wanaume ambao wanashiriki katika siku 16 za harakati za kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.
Neno “harakati” ni muhimu sana- kutakuwa hakuna mabadiliko kwenye kanuni za jijamii na kitamaduni ambazo zinaruhusu ukatili wa kijinsia bila hakati miongoni mwetu sote.
Duniani kote, makundi ya wanawake yameongoza katika kupigania na kufanya kazi dhidi ya ukatili wa kijinsia. Wanawake wakiungana kwa shughuli za kijamii, kidini na kiuchumi wanaweza kuwa na nguvu katika kuleta mabadiliko. Klabu za wasichana zinaweza kuwa na faida katika kuvunja ukimya unaozizunguka shule nyingi ambazo zinaendeleza ukatili wa kijinsia.
Wanawake wengi wa Tanzania wamefanya kampeni bila kuchoka kupigania haki za wanawake katika kumiliki ardhi na mali, kurithi katika misingi ya usawa na wanaume na kuyafikia masoko na ajira. Napenda kuchukua muda mfupi kuwasifu wanawake hawa kwa uongozi wao, kushikilia msimamo wao na kujitoa kwao. Wanatambua kwamba haki hizi za kiuchumi ni muhimu sana kama nguvu ya mwanaume na udhibiti juu ya wanawake inabidi kupunguzwa na hatimaye kuondolewa kabisa. Ni nguvu hii ambayo ndio chanzo cha ukatili unaowakabili wanawake katika maisha ya kila siku.
Hata hivyo, inaonekana wazi kuwa, kuwashirikisha wavulana na wasichana katika mkakati wa kupinga Ukatili wa kijinsia ni muhimu. Ni muhimu kwamba mbinu za kukinga zisiwachukulie wanaume kama wachochezi wa ukatili, itakuwa ngumu kubadilisha, taratibu za kijamii, na mifumo ambayo inaendeleza ukatili wa kijinsia.
Tunaendelea kujifunza jinsi ukatili dhidi ya wanawake na wasichana unaweza kuzuilika. Tunajua kwamba uhamasishaji na kampeni hazitoshi na kwamba mabadiliko yenye mageuzi yanahitajika. Mabadiliko haya yanaweza kutokea katika jamii kwa jamii zenyewe na kwamba Kivulini, Serikali ya Tanzania na serikali ya Ireland inaweza tu kuunga mkono mchakato huu.
Kama ilivyo katika bara la Afrika kwa ujumla Tanzania ni nchi yenye vijana wengi. Inakadiriwa kuwa asilimia 78 ya Watanzania wote ni chini ya miaka 35. Tanzania ijayo itajengwa na vijana wa leo. Vijana wa leo wana nafasi ya pekee kubadili sura ya Tanzania wanayoitaka. Nina matumaini kwamba hii itakuwa Tanzania ambayo itawatendea wasichana na wavulana kwa usawa na huzingatia katika kujenga maisha yenye kuthamimiwa kwa wote.
Ninatumaini kwamba ubalozi wa Ireland utaendelea kuunga mkono na kuwa pamoja nanyi katika kufanikisha hili.
Asanteni Kwa Kunisikiliza